MWANAFUNZI KATIKA NJIA ZA BWANA
0
0 Reviews 1 Orders 0 Wish listed
Tsh5,000.00 Tsh2,000.00 (Tax : )
Quantity:
Total price :
 

Sura ya 11

WOSIA WA MWANDISHI

Nikuage kwa kukwambia kwamba maisha ya utakatifu yanawezekana hata ukiwa shuleni na kwenye ngazi mbali mbali za kielimu, ijapokuwa huwa kuna changamoto nyingi sana, lakini biblia inasema tuwe waaminifu hata kufa  Ufunuo wa Yohana 2:10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

Lakini kitu cha pili nikuambie kwamba usijirahisishe kukosea, kufanya makosa ni rahisi sana ila kutubu na kurudi katika raha na bubujiko la furaha ya kimungu ni kazi sana. Jitunze jirinde na dhambi kwa gharama yoyote ile, usije ukapanga mipango ya kuingia kwenye mahusiano na binti yoyote au kijana yoyote ukijua itakuwa siri au nyie uhusiano wenu utakuwa salama kwani hamtakuja kuzini.

Ubaya  uogopee mbali sana, uzuri wowote wa sura ya mwanamke yoyote usikuvuruge kiasi cha kuacha imani, ni kweli kwamba shetani atakuwa anakuonyesha tazama yule alivyo mzuri, alafu atakwambia wai mapema wewe ili wasije waka kuwai, alafu utakuta na binti mwenyewe anatoa ushirikiano kama shetani anavyo  kusemesha. Ndugu usimkubalie shetani ni muongo sana. Mithali 1:10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Hakuna uzuri wowote ule kwa huyo kijana au kwa huyo binti, ndio maana nazidi kusisitiza kuomba sana na kujirinda na mazingira ya uovu. Ukikosa maombi kila shetani akikwambia hiki ni kizuri utamkubalia kwamba kweli ni kizuri.

Ukitaka kubisha kwamba tatizo mtumishi hujawai kukutana na warembo, wewe fanya kujaribu alafu utakuja kuona ile raha na furaha ya maisha inapotea na raha yako itakuwa ni kufanya sana zinaa au kunywa pombe ili uifanye akili ikae sawa. Utakuwa unajiuliza kwani kulikuwa na ulazima gani wa mimi hadi nikaingia katika mahusiano na huyu kijana au huyu binti, weupe wake usikuchanganye, urefu wake na misuri yake visikuchanganye, usiangalie madimpo yake au mwanya wake huyo ni shetani tu anakuchanganya kichwa ili uache wokovu huu wa thamani.

Tatizo lingine ambalo unaweza kupata ni utajikuta unakuwa mzito kufanya mambo mengi ya kimungu au kuomba maombi ya kila siku kwa nidhamu kwa sababu ya binti au kijana uliye muweka moyoni mwako kwamba mimi lazima niolewe au nimuoe huyu. Hii itakupunguzia kasi, ujasiri na hata kujiamini, automatically utajikuta kila ukimwona hamasa na nguvu za kuomba zinapungua miguuni, utakemea ilo wazo na sura yake itoke lakini haitakuwa rahisi ndio maana nimeandika sana katika kitabu hiki kwamba jiepushe sana na uhusiano na jinsia ya karibu, binti kuwa rafiki na mabinti wenzio, kijana kuwa karibu na vijana wenzio hao ndio mtendeane mema sana, msaidiane na kuwezeshana sana.

Naendelea kumcha Bwana na kuishi katika faida hizi, kwa sasa nipo naitafuta hatua ya kuingia katika ngazi za maamuzi hivyo siku yoyote ukija kuniona kwenye hatua yoyote ya juu jua nimefika pale kwa elimu na ufahamu huu nilio andika katika kitabu hiki. Ukiweza kuniombea utakuwa unafanya jambo jema ili kusudi la kuutangaza ufalme wa Mungu duniani liweze kutimia kwa wepesi.

Mawasiliano yangu yapo kurasa za mwanzoni za kitabu hiki.

Nikutakie neema ya Yesu Kristo iwe nawe ameeeen.

0

0 Ratings
Excellent
0
Good
0
Average
0
Below Average
0
Poor
0
Product Review
Product review not available
Safe Payment
7 Days Return Policy
100% Authentic Products
Sokoni Mall
0
Reviews
25
Products
More From The Store
Tsh3,000.00 Off
MWANAFUNZI KATIKA NJIA ZA BWANA
Tsh5,000.00
Tsh2,000.00
Mashine Ndogo ya kufulia na kukaushia nguo 7Kg
Tsh150,000.00
4LTR, FRIJI NDOGO YA KUBEBEKA 12V
Tsh50,000.00
Portable 12V, 8 Ltr Refrigerator
Tsh150,000.00
12V Portable electric car washer pump
Tsh180,000.00
Similar products
Tsh10,000.00 Off
Tsh60,000.00
Tsh50,000.00
Tsh500.00 Off
Tsh13,500.00
Tsh13,000.00
Top